Saturday, May 15, 2010

TANGAZO

Ndugu wadau wa libeneke hili napenda kuwafahamisha libeneke hili bado liko underconstraction ,hivyo napenda kuwaomba radhi kwa usumbufu ,lakini wote mtafahamishwa litakapokuwa hewani rasmi ,kwa utafanyika uzinduzi.
Asanteni.

Friday, April 30, 2010

MATOKEO KIDATO CHA SITA NI HAYA.

CHID WA MOSHI


Kamanda Tade kama Chid Benz.

PICHA YA UHURU PARK ITAANZA MUDA SI MREFU

Naaam ndugu zangu lile sakata la uwanja wa uhuru Park wa mjini Moshi litawajieni hapa katika blog yako ya MVUJA JASHO ,habari na picha kile kilichotokea katika baraza la madiwani wa manispaa ya Moshi.

Usikose!!!

TBL YAIPIGA JEKI TIMU YA MKOA WA KILIMANJARO.


Kaimu meneja mauzo mikoa ya Kilimanjaro na Tanga, Bw Edmund Rutaraka akiwa ameketi kabla ya kukabidhi Cash kwa viongozi wa timu ya mkoa.

Bw Rutaraka akizungumza kabla ya kukabidhi  Cash kwa timu ya mkoa wa Kilimanjaro inayojiandaa na mshindano ya Tiafa Cup.



Fedha zenyewe ni hizi nimekuja nazo taslimu sio Cheque.


Ni shilingi milioni 1.5 hizi hapa mkuu zitaisadia timu yetu.hapa akimkabidhi katibu tawala msadizi huduma na miundo mbinu Bw Hassani Bendeyeko .huku zoezi hilio likishuhudiwa na kaimu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro Darabu M Darabu na katibu wake Benedict Macha.

Sunday, April 25, 2010

NAKAAYA SUMARI AKIWA NA KINABO WA Tz Daima.

Nakaaya Sumari akiwa na mchambuzi wa masuala ya siasa na mwandishi wa habari Edward Kinabo

Saturday, April 24, 2010

WAASISI WA STYLE YA KIDUKU TZ.


Jamani hii style ya KIDUKU inayochezwa sana hivi sasa na vijana haikuanza jana wala leo ni yamuda mrefu.Hawa jamaa ndio wanastahili kuenziwa kwa sabu wao ndio waanzilishi na wana hati miliki COSOTA ya style hiyo ilikuwa ni mwaka 2003 wakati wanachukua DIP ya Jounalism pale Chuo cha TIME.
Shoto ni Abdalah Hussein maarufu kama Master Voice aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio One Sterio,kati ni Alex Malima jamaa ni askari jeshi na hivi karibuni karudi toka Dafur Kulia ni Yusuph Masanja au Masanja Junior mchizi anachukua Jiwe pale Muccobs.hapa ni kiduku kwenda mbele.

JK AMJULIA HALI KIMARO


Rais Jakaya Kikwete akizungumza akimjulia hali Mbunge wa Vunjo(CCM) Aloyce Kimaro (kushoto) aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam baada ya kuugua shinikizo la damu juzi akiwa bungeni mjini Dodoma .


Hellen Dausen ndiye Miss Universe Tanzania 2010.


Miss Universe 2010 Hellen Dausen 23 kutoka Mkoani Arusha akipunga mkono baada ya kutawazwa Malkia wa taji hilo nchini usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Warembo wakicheza Show ya ufunguzi iliyoongozwa na Nakaaya Sumari.




Hellen alipopanda kwa mara ya kwanza jukwaani.

Bofya hapa.








Friday, April 23, 2010

KIDUMU NA JD NDANI YA BONGE LA COLLABO

Mapenzi bila visa na mikasa ni mapenzi yaliyokosa chachu.Ni kama vile maisha yasiyo na kupanda wala kushuka.Yanakosa msisimko au kwa kizungu wanasema ‘boring”.Lakini inakuwaje kama visa na mikasa katika mapenzi baina ya wawili yanakuwa yamejaa visa vya kudanganyana,kunyanyasana,kutoheshimiana? Mbaya zaidi ni kwamba visa na mikasa hiyo haina mapumziko.Kila kukicha kuna msala mpya.Ukiambiwa usamehe utakubali?Ukiambiwa vumilia tu utakubali?Ukipewa ahadi kwamba “nitajaribu” kufanya au kuwa sahihi utaiamini?
Maudhui kama hayo ndiyo yaliyomo katika wimbo mpya kutoka kwa mwanamuziki maarufu Jean Piere aka Kidum kutoka nchini Burundi akishirikiana na mwana wa kwetu,Lady JayDee au ukipenda Judith Wambura.Wimbo umesimamiwa na Hermy B kutoka B’Hits Music Group ambaye hii ni mara yake ya kwanza kufanya kazi na Kidum ingawa ameshafanya kazi kadhaa na Lady JayDee zikiwemo nyimbo Mtarimbo Doro na Teja.
HABARI ZAIDI BOFYA bongocelebrity



Mapenzi bila visa na mikasa ni mapenzi yaliyokosa chachu.Ni kama vile maisha yasiyo na kupanda wala kushuka.Yanakosa msisimko au kwa kizungu wanasema ‘boring”.Lakini inakuwaje kama visa na mikasa katika mapenzi baina ya wawili yanakuwa yamejaa visa vya kudanganyana,kunyanyasana,kutoheshimiana? Mbaya zaidi ni kwamba visa na mikasa hiyo haina mapumziko.Kila kukicha kuna msala mpya.Ukiambiwa usamehe utakubali?Ukiambiwa vumilia tu utakubali?Ukipewa ahadi kwamba “nitajaribu” kufanya au kuwa sahihi utaiamini?
Maudhui kama hayo ndiyo yaliyomo katika wimbo mpya kutoka kwa mwanamuziki maarufu Jean Piere aka Kidum kutoka nchini Burundi akishirikiana na mwana wa kwetu,Lady JayDee au ukipenda Judith Wambura.Wimbo umesimamiwa na Hermy B kutoka B’Hits Music Group ambaye hii ni mara yake ya kwanza kufanya kazi na Kidum ingawa ameshafanya kazi kadhaa na Lady JayDee zikiwemo nyimbo Mtarimbo Doro na Teja.
HABARI ZAIDI BOFYA bongocelebrity

JOYCE KIRIA NA EMPTYSOULZ KUNA NINI ?

 Joyce Kiria


Ile "ndoa" kati ya kipindi maarufu kinachorushwa EAtv kinachodili na superstars wa Movies za kibongo na kampuni iliyokuwa inatengeneza kipindi hicho EmptySoulz Production chini ya Osama imefika mwisho.



Mpaka sasa blog ya “WAVUJA JASHO” haijapata "chanzo" kilichotokea kati ya kampuni inayomiliki kipindi hicho(Local Movies)  na EmptySoulz Production.Kipindi hicho ambacho awali kabla hakijaanza kutengenezwa na EmptySoulz kilikuwa kinatengenezwa na Screen Media hivi sasa kinatengenezwa na PiliPili Entertainment na episode ya kwanza ya Pilipili Entertainment imeanza kuonekana j5 ya juzi .

SIWAELEWI HAWA JAMAA KWA KWELI KUNA UNDUGU NINI ?

Naombeni mnisaidie wadau wangu inawezekana sijafahamu vizuri kuhusiana na hawa jamaa wawili kama vile wanafanana embu nisaidie na wewe kwa hili au ni macho yangu. Hapa ni R .Kelly na Avant.gonga comment zako hapa.

HASHEEM THABIT IS BACK HOME


Ebwana kama kawaida mie natupia kati mpango huu ,jana mchizi wangu alikuwa town katika pitapita zake kwenye foleni zetu za mataa ya jiji la Dar ilipaki gari moja ya maana sana,achana na hivi  Vi  Range Rover Sport vilivyojaa hivi sasa town vya milioni 45 hadi 50,ilipaki bonge la Range Rover Vogue halisi ya "ukweli" yaani Kitu K  ambayo bei yake kwa harakaharaka ni kama m 250 hizi zetu za madafu ndani yake alikuwamo Super Star na mchezaji wa kikapu wa timu ya Merphis Grizzlies inayoshiriki ligi kubwa ya mchezo huo duniani ya NBA hapa namzungumzia Hasheem Thabeet Manka, jamaa akanitupia ishu hiyo kwamba jamaa kwa sasa kama vile ka back home ,itakuwa amewamisi washikaji any way karibu sana home broad.

NDANDA COSOVO ,BELLE 9 KUPAMBA ,ISS UTALII KANDA YA KASKAZINI.


Mwanamuziki machachali nchini,Ndanda Cosovo al maarufu kama KICHAA na bendi yake ya Muziki wa Dansi atatumbuiza katika shindano la kumpata Miss Utalii Vyuo Vikuu 2010 – Kanda ya Kaskazini,shindano litakalo fanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kitalii ya Naura Springs jijini Arusha ,siku ya Ijumaa Tarehe 30-4-2010.


Pamoja na Ndanda Cosovo,mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Belle 9 pia atatumbuiza katika shindano hilo sambamba na makundi ya ngoma za asili za makabila ya Mikoa ya kanda ya Kaskazini.
Ndanda Kosovo amejigamba kuwa siku hiyo wataporomosha onyesho la kihistoria nchini,na kuudhihirishia umma wa watanzania kuwa yeye na bendi yake hawana mpinzani.

Shindano hilo linaloshirikisha jumla ya warembo kumi na mbili kutoka vyuo vikuu vilivyopo kanda ya kaskazini,litatoa washindi ambao watawakililisha Vyuo Vikuu vya Kanda ya Kaskazini katika fainali za Taifa ya Miss Utalii Tanzania 2010 zilizopangwa kufanyika mwezi Julai 2010 jijini Dar Es Salaam.

Warembo katika shindano hilo watapita jukwaani na mavazi ya Ubunifu .Kitalii,Kutokea na mavazi ya asili.pia warembo hao watashindana kuwania tuzo ya Miss Utalii Vyuo vikuu Kipaji,kwa kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili ya makabila ya Tanzania.

Tanzania katika mashindano hayo inawakilishwa na warembo wawili wa Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu 2009,ambao ni Romery Zahoro toka chuo cha Usimamizi wa Fedha na Zakhia Omary toka chuo kikuu cha Dar Es Salaam.

Thursday, April 22, 2010


HAJAWAHI CHAGULIWA HATA MARA MOJA KUGOMBEA TUZO...ILA MWAKA HUU YUMO..



>>>MPIGIE KURA KATIKA KILI MUSUC AWARDS 2010 KUPITIA WIMBO WAKE WA MUNGU YUKO BUSY.


KUMPIGIA KURA:-andika kilim56 kisha tuma kwenda namba 15723<<<

TAYARI AMEKWISHA ACHIA KAZI YAKE MPYA MWAKA HUU WA 2010 INATAMBULIKA KAMA "HUWEZIJUA"AKIMSHIRIKISHA MTUMZIMA KUTOKA CALIF...JUA CALI...GOMA LINABAMBA NA LINAKIMBIZA KWASASA ON RADIO STATIONS ALL OVER EAST AFRICA....JIONGEZE HAPO DOWN KUNA LINK YA KUDOWNLOAD NGOMA ZA MISOSI IKIWAMO NA HIYO MPYA"HUWEZIJUA".


NEMLESS ATUA BONGO TAYARI KWA MAKAMUZZZZZZZ


Nyota wa muziki wa kisasa "Bongo Fleva kutoka Kenya Nameless (kulia) akiwa na Nyota Mwenzake wa Tanzania AY muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam leo. Nemeless ni mmoja wa wasanii watako tumbuiza katika shindano la Miss Universe Aprili 23, 2010 katika ukumbi wa Mlimani City.


Ofisa wa kampuni ya Compass Communications, Mwanakombo Mjajukiakimkaribisha msanii kutoka Kenya Nameless muda mfupi baada ya kuwasilikatika Uwanja wa Ndege was Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo .


                                                         Kwa taarifa zaidi Bofya hapa
                                 http://mrokim.blogspot.com/


RAPPER MWINGINE AFARIKI DUNIA...

PIMP C


Siku chache baada ya kuripotiwa kwa taarifa juu ya kifo cha Rapper mkongwe na memba wa kundi la Gangstarr GURU,Rapper mwingine PIMP C(pichani juu) naye amaefariki dunia akiwa kwenye chumba cha hotel aliyofikia,imeripotiwa kuwa mtu mmoja alipiga no 911 na L.A Country Fire kumkuta amelala juu ya kitanda chake akiwa tayari ameshakata roho.

PIMP C ambaye jina lake halisi ni Chad Batler alikuwa mmoja kati ya memba wawili wa bendi ya Hiphop ijulikanayo kama UGK,bendi ambayo ilijichukulia umaarufu sana baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Jay Z "Big Pimpin" mwaka 2000,mara ya mwisho walionekana kwenye video ya wimbo wa OutCast "International Player Anthem(i choose you)".

Perfomance ya mwisho ya mshkaji huyu ilikuwa pamoja na rapper mwingine Too Short na ilifanyika pale House of Blues L.A jumatatu ya wiki hii.R.I.P brother.



RAPPER GURU KATUTANGULIA...


Wiki hii nikiwa kwa Lukuvi nilishituka sana na siku yangu kuharibika baada ya kupokea ujumbe mfupi kutoka kwa mchizi wangu akinifahamisha kuwa rapper wa kundi la Gangstarr GURU(43) aliyekuwa akisumbuliwa na Saratani kuwa hatuko naye tena!,Rapper huyu alikuwa akiheshimika sana alifariki dunia january 19 asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu na alikuwa  akirudirudi kwenye koma mara kwa mara,Producer Solar alisema mchizi aliugua sana kwa takribani mwaka mzima na madaktari bingwa wamejitahidi sana kuokoa maisha yake lakini inaoneka kama MUNGU kampenda zaidi yetu,tutamkumbuka sana mchizi kwa ngoma kali,flows za ukweli na rylics za maana,"GURU umeondoka wewe lakini umetuachia ngoma zako kibao ambazo tutazitumia kukukumbuka".
R.I.P.

Ricaldo Kaka akumbuka siku aliyovishwa nepi?

Leo April 22 ni Birthday ya huyu jamaa ambaye alikuja duniani siku kama ya leo mwaka 1982, Nyota huyu anakipiga klabu ya Real Madrid ya Hispania na Brazil akiwa anatetea taifa lake,ukimtazama mgongoni wakati amevalia jezi yake kuna namba 8.Kama unasheherekea birthday yako leo basi unasherekea na superstar huyu wa soka.Blog ya burudani inawatakia wale wote wanasherehekea birthday zao leo Happy birthday.

Monday, April 12, 2010

WASHINDI PROMOSHENI YA KWEA PIPA WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO.


Dixon Busagaga wa globu ya BO akiwa ameshikilia jembe kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhizawadi kwa washindi wa promosheni ya Kwea Pipa. 

Baadhi ya viongozi wa Bonite kutoka Shoto meneja Uajili Dominic Urasa,Meneja tawi la Arusha, Mongola Segule, Meneja wa fedha Gidion Kaaya,Meneja Masoko Gilbert Uisso na Meneja mauzo wa kiwanda hicho Christopher Loiruk

Uiso akinywa coca cola baada ya kuwaambia watu waliofika kwenye hafla hiyo kuwa mbali na zawadi pia utaendelea kuburudika na kinywaji chako.

Mshindi wa wa tiketi katika promosheni ya Kwea Pipa Saimoni Makao akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tiketi yake.
Meneja Masoko kiwanda cha Bonite Girbert Uiso aksoma majina ya washindi wa Tiketi na TV katika Promosheni ya Kwea Pipa na ushinde.

Meneja uajili wa kiwanda cha Bonite Dominick Urasa akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa zawadi ya TV katika promosheni ya Kwea Pipa Juvina Mwita


Meneja wa fedha kiwanda cha Bonite Gidion Kaaya akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa zawadi ya tiketi ya promosheni ya Kwea Pipa Saimon Makao.



baadhi ya washindi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Kwea Pipa.

Hizi bado zipo nyingi kama vipi funuwa vizibo kadri uwezavyo dukani inauzwa laki tisa.kwenye Promosheni ni mia 4 tuuu.

TV kubwa aina ya BRAVIA pia zilitolewa kwa washindi sita

Dixon Busagaga wa bog ya BO akiwa na mshindi wa tiketi katika promosheni ya Kwea Pipa Saimon Makao mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake .

Friday, April 9, 2010


Mshikaji akiwa kwenye kazi kidogo mzaha anaweka kando kwa vile tuu anajua yupo hapo kwa ajili ya wateja wake yaani wasikilizaji wake,Ukikutana nae street hutoweza amini kama ndivyo alivyo kutokana nauwezo wake wa kujibadilisha kulingana na maeneo aliyopo wakati huo,,Kijana ni mjita toka pande za Musoma anajivunia kuwa kijana pekee aliye adopt kabila na dini ya Mama yake ,huyu ndiye yule bhajamen bhajamen haka kajamaa Mwili mdogo,umri mdogo lakini kakiingia kwenye ri radio eti kana jiita DDDDDDJAY CLEVER.
Mchizi anaonekana ni Multiple  maana hadi sasa haijafahamika kipaji chake cha ukweli ni kipi,kwako wewe ambaye hujui kuhusu kijana huyu ni kwamba jamaa ni Presenter  wa radio,ni Dj,jamaa ni mwandishi wa habari anapiga Artical za kufa mtu kwenye Gazeti la Tz daima,mchizi ni mwanaspoti na pia jamaa ni Photographer anakamua video na still pix.
Huyu si mwingine ndiye Dixon Busagaga mjukuu wa bibi pili.
anakamua vipindi hivi.The base ,Midmorning crues,The project 120,The Magic weekend na EXTRA BASE ya kila jumamosi saa 9 mchana,sooo mnakaribishwa sana 
Jamani ndugu zangu karibuni mjengoni ,kuta nne zimenitawala hapa ndani nasikia harufu ya kiyoyozi peke yake.
Vipi tena hapa mbona kama vile kidume mimi sipaelewi saa haisomo ,computer haihemi ni mkono wa mtu nini?
Mhh ngoja nicheki pande hii kama vile stimu haijalipiwa vile ningojeni kidogo watu wangu!
Ina scratch hii mbona sisikii!
dj clever mazoezini.
Huyu jamaa anafanya utaratibu wa kuvaa Joho hapo Muccobs lakini kama unayovyofahamu mja haachi asili
mbali na kitabu pia anaendeleza kipaji anakamua bonge la shoo siku ya jumapili majira ya saa 5 hadi saa 6,sho inakwenda kwa jina la MOVEMENT AMPLIFIED huko ndani kuna vyombo kibao si vya kitoto,mshikaji ana asili ya kabila linaloongoza kwa kula Ugali,kama vile msukuma lakini mwenyewe ukimuuliza anasema yeye na AKON ni mtu na bro wake yaani ni Msenegar.anajiita Masanja Junior ingawaje kwenye cheti chake cha vidudu kuna jina la Yusuph Mazimu.waweza mcheki hapa pia http/www.mazimu11.blogspot.com

Uisikia MZEEEIYAA MZEEIYAA huyu ndiye mwenye,jina hilo linafahamika sana kwa vijana wa kiume kwasaaana wa kike pia ,wakati mwingine baadhi ya wati wenye jina kama leke huko mitaani na wao wamejipa jina hilo ili wawang'oe kina dada wenye shobo kirahisi,yeye pia ana tokea Vudee ni kijana wa Kipare amekulia katika kata yenye watoto wengi kuliko kata nyingine nikiwa namaana ya PASUA maarufu ka 'PS',jina lake la kwenye ATM card yake ni Emmanuel Mzava,ukifungulia radio yako saa 8 mchana utasikia sauti yake,anafanya vizuri sana kwenye THE BASE,MOSHI FM COUNT DOWN,na kipindi chenye mashabiki lukuki cha The Mirdmorning Crues akiwa na swahiba wake Dixon Busagaga.
Huyu jamaa ndiyo yule mara kwa mara wenzake wanamuita kiboko lakini yeye anajiita Mchezaji nguli na pengine mkongwe kuliko wote,mkewe nyumbani anamuita Hafidh,mtaani wanamuita Kipese ,bosi wake anamuita Henry Limo.kama unavyomuona mwanya wake yeye ndio identity yake hapa kama kawaida alikuwa akiendesha kipindi cha michezo ambacho ni bora kwa kanda ya kaskazini ,ANGA LA MICHEZO.

Kikosi kazi cha Radio makini yaani Moshi fm.

Huyu ni Helen Msumba binti wa kipare mwenye sauti kama vile nzito fulani hivi ,hapa alikuwa akiendesha moja kati ya vipindi anavyofanya kipindi cha Life Acces,hapa masuala yoooote ya maisha utapata kuyasikia,shoto ni Asia Msangi akimpa ubavu kwa tabasamu.

Thursday, April 8, 2010

KARIBUUUUUU SANAAAAAAAA

Sunday, April 4, 2010

KILIMEDIA F.C HUREEEEE HUREEEEEE

kikosi cha kili media tayari kwa ajaili ya maandalizi ya kambi.


Baadhi ya wachezaji wa timu ya Kilimedia f.c wakiwa katika uzi muda mchache baada ya kukabidhiwa jana ,uzi huo umetolewa na mdau wa michezo mkoa wa Kilimanjaro Fraji Swai ambaye pia ni mkurugenzi wa Kilimanjaro Aids Contral Association.kutoka shoto ni Rodrick Mushi(Tz daima),Nakajumo James(Mtanzania)Dixon Busagaga(Radio Moshi fm) Kijah Elias (Star tv) na Zephania Endrew (RFA)

Chukueni vifaa vijana mkaanze kazi....haya ni maneno kutoka kwa mwenyekiti.
















Sasa kaianzeni kazi .....Kaimu mwenyekiti wa baraza la wazee manispaa ya Moshi ,Abdalah Kimweri akimkabidhi katibu wa muda wa Kilimedia f.c NAKAJUMO JAMES.Vifaa vya michezo vyenye thamani ya kiasi cha shilingi  M 1.Shoto ni mkurugenzi wa KACA ,FARAJI SWAI ambao ndio watoaji wa vifaa hivyo.