Mwanamuziki machachali nchini,Ndanda
Cosovo al maarufu kama KICHAA na bendi yake ya Muziki wa Dansi atatumbuiza
katika shindano la kumpata Miss Utalii Vyuo Vikuu 2010 – Kanda ya
Kaskazini,shindano litakalo fanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kitalii ya Naura
Springs jijini Arusha ,siku ya Ijumaa Tarehe 30-4-2010.
Pamoja na Ndanda Cosovo,mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Belle 9 pia atatumbuiza katika shindano hilo sambamba na makundi ya ngoma za asili za makabila ya Mikoa ya kanda ya Kaskazini.
Ndanda
Kosovo amejigamba kuwa siku hiyo wataporomosha onyesho la kihistoria nchini,na
kuudhihirishia umma wa watanzania kuwa yeye na bendi yake hawana mpinzani.
Shindano hilo linaloshirikisha jumla ya warembo kumi na mbili kutoka vyuo vikuu vilivyopo kanda ya kaskazini,litatoa washindi ambao watawakililisha Vyuo Vikuu vya Kanda ya Kaskazini katika fainali za Taifa ya Miss Utalii Tanzania 2010 zilizopangwa kufanyika mwezi Julai 2010 jijini Dar Es Salaam.
Warembo katika shindano hilo watapita jukwaani na mavazi ya Ubunifu .Kitalii,Kutokea na mavazi ya asili.pia warembo hao watashindana kuwania tuzo ya Miss Utalii Vyuo vikuu Kipaji,kwa kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili ya makabila ya Tanzania.

Tanzania
katika mashindano hayo inawakilishwa na warembo wawili wa Miss Utalii Tanzania
Vyuo Vikuu 2009,ambao ni Romery Zahoro toka chuo cha Usimamizi wa Fedha na
Zakhia Omary toka chuo kikuu cha Dar Es Salaam.
0 comments:
Post a Comment