Mapenzi bila visa na mikasa ni mapenzi yaliyokosa
chachu.Ni kama vile maisha yasiyo na kupanda wala kushuka.Yanakosa msisimko au
kwa kizungu wanasema ‘boring”.Lakini inakuwaje kama
visa na mikasa katika mapenzi baina ya wawili yanakuwa yamejaa visa vya kudanganyana,kunyanyasana,kutoheshimiana?
Mbaya zaidi ni kwamba visa na mikasa hiyo haina mapumziko.Kila kukicha kuna
msala mpya.Ukiambiwa usamehe utakubali?Ukiambiwa vumilia tu utakubali?Ukipewa
ahadi kwamba “nitajaribu” kufanya au kuwa sahihi utaiamini?
Maudhui kama hayo ndiyo yaliyomo katika wimbo mpya
kutoka kwa mwanamuziki maarufu Jean Piere aka Kidum kutoka nchini Burundi
akishirikiana na mwana wa kwetu,Lady JayDee au ukipenda Judith Wambura.Wimbo
umesimamiwa na Hermy B kutoka B’Hits Music Group ambaye hii ni mara yake ya
kwanza kufanya kazi na Kidum ingawa ameshafanya kazi kadhaa na Lady JayDee
zikiwemo nyimbo Mtarimbo Doro
na Teja.
HABARI ZAIDI BOFYA bongocelebrity